SIMBA YATAMBA, KABURU ASEMA LIWAKE JUA, IPIGE MVUA POINTI TATU LAZIMA.





 Na  Melkiory Gowelle.

MAKAMU wa Rais wa Simba FC Geofrey Nyange Kaburu ‘Perezi’ ametamba kuwa lazima wataibuka na ushindi wa pointi tatu katika mtanange wao dhidi ya Kagera Sugar utakao pigwa katika dimba la Kaitaba Mkoani Kagera wikiendi ya jumapili hii.

Akizungumza Mkoani Kagera Kaburu amesema kikosi kimekamilika na kipo tayari kuwakabili wenyeji wao sababu wachezaji wote nane waliokuwa wakizitumikia timu zao za Taifa akiwemo Mrundi Laudit Mavugo wamesha tuwa katika ardhi ya Kagera tayari kwa mapambano.

“Tunashukuru Mungu tumefika salama, tayari kabisa kupambana na kuvuna pointi tatu muhimu katika uwanja wa kaitaba, tumekuja wachezaji nane na mimi wa tisa moja kwa moja wataingia katika ‘programu’ na mwalimu, hivyo pointi tatu ni muhimu, liwake jua inyeshe mvua". amesema Kaburu.


Simba wapo katika mbio za ubingwa wakiwa kileleni kwa jumla ya pointi 55, nyuma ya mahasimu wao Yanga wenye pointi 53 wote wakiwa wameshuka dimbani mara 24.
Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment