JE WAJUA KUWA NGUO YA KITENGE HAIMCHUKIZI MTU



Na Anna Richard
KITENGE ni moja ya vazi la kitamaduni katika nchi nyingi za kiafrika lililo jitengenezea umaarufu mkubwa duniani kote pia.Nchini Tanzania, vitenge huwa vinavaliwa sana hasa nyakati za shughuli kama kichenparty ,harusi nk.

Vazi la kitenge hapo awali lilizoeleka kama ni vazi la wakina mama tu lakini kwa sasa vazi hilo limeonekana kuwa na soko sana kwa wakina dada yani kwa mabinti. 

Lakini kitenge pia hutumika kutengeneza nguo nyingine tofauti kwa kushona ukiwatumia mafundi nguo.

Mara nyingi kitenge huwa hakimchukizi mtu inategemea wewe na mshono ulio amua kuushona lakini pia rangi ya kitenge chako hukufanya uvutie inategemea na rangi ipi umeichagua.
Wanawake wengi hupenda kushona magauni ya kitenge kwasababu unakuwa na uwezo wa kuweka mtindo wowote unaotaka lakini pia si gauni pekee Ata sketi na blauzi ,suruali  na makoti vyote ivyo unaweza ukavishona kwa mtindo unao upenda wewe.
Lakuzingatia hakikisha unapata kitenge kizuri na kinacho endana na rangi ya ngozi yako, lakini pia hakikisha Fundi unae mpa nguo yako akushonee, ni mwaminifu na anae fanya kazi yake kwa ufasaha zaidi.


 
Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment