Na Melkiory Gowelle
Wasanii wa
filamu nchini, wametakiwa kupambana katika kutengeneza kazi zenye viwango ili
kuwarudisha Watanzania katika soko lenye ubora wa hali ya juu kama ilivyokuwa
hapo awali.
Wito huo
umetolewa leo Jijini Dar es salaam na msanii mkongwe wa tasnia hiyo bongo,
Vicent Kigosi ‘Ray’ katika kipindi cha
Jahazi kinacho rushwa na Clouds fm.
Ray amesema
kuwepo kwa utitiri wa filamu za kibongo zilizokosa ubora katika soko,
kumesababisha kupanda kwa thamani ya filamu za kigeni zikiwemo za kizungu na zakikorea.
“Unajuwa sehemu
yeyote yenye biashara basi kila mtu anataka kuingia ili afanye biashara bila
kuzingatia viwango na ubora wa biashara hiyo. ” alisema Ray.
“Sasa hivi
Watanzania wameamka, kwahiyo tengeneza kitu kizuri watu watakichukuwa tu,
sawasawa na kupika chakula kizuri
ambacho watu lazima wale.” Aliongeza Ray.
Ray amepania kurudisha hadhi ya filamu za Kitanzania kupitia filamu yake mpya iitwayo 'GET KIPPER' inayo tarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment