TEMBELE AFUNGUKA MAZITO KUHUSU YANGA, AWATAKA VIONGOZI NA WADAU WA SOKA KUZINGATIA HAYA.

Na. Melkiory Gowelle




Mabingwa mara mbili mfululizo wa Ligi kuu Tanzania bara, Young Africans SC, wamejikuta katika ‘alarm’ ya mpasuko mara baada ya kukumbwa na mtikisiko mkubwa wa kiuchumi ndani ya club.


Akielezea kinaga ubaga sababu za hali hiyo, mchezaji nguli wa zamani wa timu hiyo Ally Mayayi ‘Tembele’ amekiri kuwa hayo yote yanatokea kwasababu ya matatizo yanayo mkabili Mwenyekiti wa timu hiyo Yusuph Manji.


Akizungumza Jijini Dar es salaam Tembele amesema “ni kweli kabisa kuwa kinacho mtokea Mwenyekiti , kina mahusiano makubwa na kinachoitokea timu kwa hivi sasa”

“Ndugu Manji baada ya kukabidhiwa timu kama Mwenyekiti, haikuwahi kutokea kwa matatizo ya mishahara wala namna ya uendeshaji wa timu, tofauti na ilivyokuwa sasa.” Alisema Tembele.


Aidha Tembele amesema kuwa kila kitu mahali popote katika maisha huwa kinatokea kama funzo, hivyo ni wakati kwa wadau wa michezo kujifunza toka kwa Yanga.


Katika hatua nyingine Tembele amewataka viongozi na wachezaji wa timu hiyo, kukaa pamoja na kuangalia matakwa ya timu ili kuikabili hali ya ushindani katika mechi zao za kitaifa na kimataifa.

“pamoja na kinachotokea ni lazima viongozi na wachezaji wahakikishe kwamba haya matakwa ambayo ni malengo ya timu na mahitaji ya wanachama wanayatimiza kama yalivyo pangwa.” Alisema Tembele.



Ikumbukwe kuwa tangu Yusuph Manji awe Mwenyekiti wa  Yanga 2006, timu hiyo imefanikiwa  kushinda mataji takribani 10, yakiwemo 7 ya ligi kuu, 2 ya kagame na 1 la FA,  na kuweka rekodi ya kuwa timu pekee Tanzania bara inayo lipa mishahara minono kwa wachezaji na viongozi wake.

Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment