NDOTO ZA YANGA KUHAMIA KIRUMBA ZAYEYUKIA DAR.



Na.Melkiory Gowelle.
MABINGWA watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara ‘VPL’Young African Sports Club wanatarajia kushuka dimbani April 8, 2017 kukipiga dhidi ya MC Alger ya Algeria katika mechi ya kimataifa ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Awali taarifa za uhakika toka katika uongozi wa klabu hiyo, zilieleza kuwa mtanange huo utapigwa katika dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza, lakini kwa sasa zoezi hilo limeshindikana na wamejikuta wakirudi katika uwanja wao wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza Jijini Dar es salaam katibu mkuu wa Klabu hiyo Charles Bonifac Mkwasa ‘Masta’ amesema kuwa sababu kubwa ya kukwama kwa zoezi hilo ni marekebisho ya uwanja wa CCM Kirumba pamoja na sheria na taratibu za michuano hiyo.


“Ni kweli tulipanga kucheza Mwanza, kutokana na Yanga kuwa na idadi kubwa ya wapenzi hasa kanda ya ziwa. hivyo tulitaka tukatoe burudani kwao, lakini hali ya uwanja bado inafanyiwa marekebisho, pia sheria za michuano hii zina sema ndani ya siku 20 timu zote mbili zina takiwa zitambue uwanja watakao tumia na muda utakao chezwa, hivyo jaribio hilo limeshindikana”.  Amesema Mkwasa.

Aidha Mkwasa amekanusha taarifa zinazo dai kuwa walitaka kubadilisha uwanja kutokana na matokeo mabaya waliyo yapata katika mechi za kimataifa zilizochezwa hivi karibuni katika uwanja huo.

“Tuliona ni vyema mechi hii tuipeleke mikoani ili tukawape burudani wapenzi na wanachama wengine wa Yanga, si kweli kuwa tunakimbia uwanja ili tupate matokeo, wakati tumesha pata matokeo mengi na mazuri wakati tukicheza hapa. Tuliwafunga Fc Platinum bao 5-0 hapa hapa.

Yanga wamejikuta katika Kombe la Shirikisho mara baada ya kushindwa kufurukuta katika Michano ya Klubu bingwa dhidi ya Zanaco Fc ya Zambia, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 uwanja wa Taifa na matokeo ya 0-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa Jijini Lusaka nchini Zambia ambapo Zanaco walisalia katika michuano hiyo kwa faida ya goli la ugenini walilo lipata.,

Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment