Na, saphinia seleman.
Baada ya Waziri Mkuu wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa kassimu Majaliwa kupiga marufuku
pombe aina ya viroba, wananchi wameanza kutekeleza agizo hilo.
Mh, Majaliwa alitangaza rasmi
ifikapo tarehe 1 mwezi wa tatu 2017 pombe hiyo isionekane mitaani na yeyote
atakaebainika kutumia kilevi hicho atapigwa faini ya shilingi elfu 50000.
Tamko hilo limeleta mtazamo
chanya kwa wananchi wa mtaa wa mbezi beach "A "makazi mapya
ambapo wamekubaliana na agizo la Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wa
habari mjumbe wa mtaa huo bi, Mwajuma Mnamba amesema atafuatilia kuhakikisha
kila mmoja anazingatia agizo hilo.
0 comments:
Post a Comment