BAO LA AJIBU LAMPA UTATA NGASSA




Na Abdul Claus

BAO  la kwanza la kusawazisha lililo fungwa na mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib katika mchezo Wa VPL dhidi ya Mbeya city uliopigwa Wikiendi hii  limemwacha katika hali ya sintofahamu Kiungo mshambuliaji wa mbeya City Mrisho Ngassa(Pichani kushoto).

Mchezaji huyo mkongwe Katika VPL ametupia lawama maamuzi ya maamuzi wa mchezo huo
Akizungumza na chombo kimoja cha habari Ngassa aliweka wazi kuwa mkwaju wa adhabu uliosababisha goli hilo haukuwa wa halali.

"Ukiangalia ile faulo Aliyopiga Ajibu Siku ile ya mchezo wetu na Simba  ikawa goli haikuwa halali kabisa kabisa kwasababu beki wetu alikwenda kucheza mpira ila Mo ibrahimu akajiangusha na maamuzi akatoa faulo kwa lakini kwa upande wa Penati yao sina wasiwasi nayo ilikuwa ni halali".


Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment