JE UNA SHEREHE NA HUJUI UTOKE VIPI





Na mwanahawa sabasi 
Wakati mwingi wanawake hupata wakati mgumu kuamua wavae mavazi  gani­­ ­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­­katika hafla au sherehe.
 Ugumu huo hutokea hasa kwenye sherehe ikiwa ya ghafla hivyo humfanya muhusika kutokupanga mapema muonekano wake wa siku hiyo .
Wengi wamekua wakijikuta wanatumia pesa nyingi kutafuta uvumbuzi wa haraka wakati inawezekana kabisa  kukabiliana na hali hiyo kama utakua umejiwekea utaratibu mzuri,wa
Kukabiliana na tatizo hilo mwanamke anashauriwa kuwa na nguo maalumu kabatini ambazo unaweza kuzivaa kwa ajili ya matukia kama hayo .
 Ni muhimu kwa mwanamke kuwa na magauni marefu na yenye mvuto  ambayo yatakuwezesha kuingia popote na kuvutia hata kama hajajiremba sana.   
 Endapo utakua na nguo za namna hizo utakua na urahisi wa kufanya uamuzi wa haraka na bado ukaonekana mwenye mvuto.
Hakikisha ndani kwako  kuna vipodozi vyote vya muhimu ambavyo vitatumika kwenye kujipodoa na kubadili muonekana wako. 
Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment