MV UMOJA MBIONI KUKAMILIKA




Na Fatuma Kitima,Dar es Salaam
SERIKALI imesema kuwa kukamilika kwa ukarabati wa meli ya MV Umoja kutarudisha huduma ya usafirishaji wa mizigo katika kanda ya ziwa kupitia bandari ya Kemondo  iliyopo mkoani Kagera  ambayo itabeba mizigo  ya  mabehewa na reli.
Sambamba na kukamilika kwa ukarabati huo ,Serikali imeagiza Shirika la reli Nchini (TRL) kufanya ukarabati wa reli haraka  ili kuepuka usumbufu wakati wa kushusha na kupakia mizigo .
"TRL haina budi  kufanya ukarabati njia za reli bandarini haraka iwezekanavyo ili kuruhusu mizigo itakayokuja ikiwa kwenye mabehewa kwa njia ya meli iweze kupakuliwa wakati Meli itakaposhusha " amesema
Taarifa hiyo imetolewa wakati wa ukaguzi wa bandari hiyo, na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amesema kuwa,  kukamilika kwa ukarabati wa meli ya MV Umoja kutarudisha huduma ya usafirishaji wa mizigo katika kanda ya ziwa kupitia bandari hiyo.
Pia ameitaka  Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Shirika la Reli Nchini (TRL), na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL),  kuanza kuandaa Mfumo mmoja wa kutoa Stakabadhi ili kuwarahisishia wateja wake huduma za usafirishaji wa mizigo.
Ametoa  wito kwa  Mamlaka hiyo kuanza kutafuta tena wateja ambao kwa muda mrefu walikuwa wamepotea kutokana na  bandari hiyo kusuasua kutoa huduma zake kwa muda mrefu.
Naye  Meneja wa TPA Kanda ya Ziwa Bw. Abel Moyo, amemuahidi Waziri huyo  kutekeleza agizo lake kwa kushirikiana na TRL pamoja na MSCL na kuwahakikishia wafanyabiashara wa kanda ya ziwa  kuwa na matumaini mpya ya kupata usafiri bora na wa uhakika.

Wakati huohuo Waziri Mbarawa ametembelea na kukagua Kivuko cha Kyanyabasa kinachotoa huduma katika mto Kyanyabasa na kumtaka Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) mkoani humo, Injinia Zephrine Bahyona,  kutoa huduma bora sambamba na ukusanyaji wa  mapato ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili.
Injinia Zephrine Bahyona, amezitaja baadhi ya changamoto zinazoathiri utendaji mzuri wa kivuko hicho ni, kukatika kwa magugu maji na hivyo kupelekea kusombwa kwa kivuko.
Sanjari na hayo Waziri Profesa Mbarawa pia amekagua barabara ya Uyovu- Bwanga yenye urefu wa kilometa 45 mkoani Geita na kuridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo ambapo ujenzi wake kwa sasa umefika asilimia 56%.

Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment