Na Doroth Mnubi
Mkuu wa
idara ya masomo chuo cha uandishi wa habari TSJ Blandina Semaganga ametoa
sababu zakusogezwa mbele ziara ya wanafunzi chuoni hapo ya kutembelea vyombo
mbalimbali vya habari ambayo ilitakiwa kufanyika siku ya tar 21/3/2017 ambayo
ni kutojiandaa vya kutosha kwa uongozi wa chuo na kutota taarifa mapema kwa
vyombo husika.
" kweli jana media tour
haikuwepo kwa sababu hatukuwa na maandalizi ya kutosha kama chuo na
hatukupeleka maombi mapema kwa sababu media nazo zina ratiba zake nyingine ila
wanafunzi wasijali kwa kuwa tumesogeza mbele hadi tar 10/4/2017 baada ya
siku ya bash itakayo kuwa siku ya ijumaa jumatatu yake ndio itakuwa media tour
kwahiyo wanafunzi wajiandae tu"amesema madam semaganga.
Pia aliongezea kusema kuwa wanafunzi
wazidi kusoma kwa bidii katika masomo yao ili waweze pata GPA nzuri ambazo
zitawasaidia kuendelea na elimu ya juu.
0 comments:
Post a Comment