SIMBA WAKALIA KUTIKAVU


 NA TUZO MAPUNDA.
Timu ya Simba klabu  imelazimisha sare ya 2-2 na Timu ya Mbeya city katika Ligi kuu Tanzania bara.
Mechi hiyo ilipigwa leo katika uwanja wa taifa Dar es salaam,ambapo timu ya Simba ili kuwa mwenyeji wa mchezo huo.
Mpira ulianza kwa kasi uku kila timu washambuliaji wake wakiwa na uchu wa kushambulia lango la mwingine hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Timu ya mbeya city ilikuwa imetangulia mbele kwa goli 1-0  dhidi simba goli likifungwa na Ditram Nchimbi mnamo dakika ya 37akipokea pasi safi kutoka kwa Ngassa.
Kipindi cha pili kilianza kwa washambuliaji wa simba wakishambulia lango la mbeya city ambapo mshambuliaji wa timu ya Simba  Ibrahim Ajibu aikifunga bao safi kwa kupiga mpira wa faulo baada ya Laudit mavugo kuchezewa rafu na Mabeki wa mbeya city.
Mpira uliendelea kwa kasi huku mbeya city wa kishambulia kwa kushitukiza kufikia dakika ya 78  mshambuliaji Mkemi Aliy aliiandikia timu ya mbeya city bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ditram Nchimbi .
Dakika ya 84 timu ya simba ilipata penati baada ya walinzi wa timu ya mbeya city kumchezea mwamed shabalala mchezo usiokuwa  wa kiungwana ambapo Shiza kichuya aliifungia simba bao la pili.
Hadi mchezo unamalizika dakika 90 timu zilitokana uwanjani zikiwa zimetoshana nguvu ya kufungana 2-2


Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment