KADI YA CHIRWA YA ZUA UTATA


Na Abdul Claus
               Kadi nyekundu aliyopewa mshambuliaji wa klabu ya soka ya Yanga Obrey CHIRWA, Kwenye mchezo wa VPL dhidi Ruvu shooting imeibua maswli mengi kwa wadau wa soka nchini.
                    Wadau hao wameeleza kutolidhishwa Na maamuzi ya mwamuzi Simba kutoka Kagera alichezesha mchezo huo.
Akizungumza Na vyombo vya habari mara baada ya mchezo huo msemaji wa Ruvu shooting Masau Bwile ametanabaisha kutolidhishwa Na maamuzi ya Simba hususani kadi nyekundu aliyopewa CHIRWA 

"Nikweli tumepoteza mchezo dhidi ya Yanga lakini ninawasiwasi Sana juu ya Mwamuzi Simba hakuweza kabisa kumudu mchezo mzima ukiangalia hata kadi nyekundu aliyopewa CHIRWA haikustahili kwani sikuona sehemu alishika mpira kwa mkono alifunga goli halali kwa kichwa"
Naye mwanachama wa Yanga Sanari Sanari ameitaka kamati ya masaa 72 ya TFF kuifuta mara moja kadi hiyo kwani si halali 
"Hizi ni figisufigisu tunafanyiwa mchezaji wetu hakufanya kosa lolote anapewa kadi ya njano inayopelekea kadi nyekundu Na goli halali linakataliwa, nawaomba TFF waifute kadi hiyo kama walivyofuta kadi  nyekundu ya Jonas Mkude"
Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment