Na kasabe100@yahoo.com
BENKI ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeonesha nia ya kuisaidia Serikali katika
kutekeleza miradi ya Uzalishaji na Usambazaji wa Nishati ya Umeme ili kuwezesha
kuinua uchumi wa taifa.
Hayo
yamebainishwa hivi karibuni wakati wa kikao kati ya Wizara ya Nishati na Madini
kikiongozwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Medard Kalemani, Watendaji wa
Wizara
na
Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Wakurugenzi Watendaji 12
wanaowakilisha nchi zao katika benki hiyo.
Akizungumzia
ushiriki wa benki hiyo katika kusaidia kuendeleza sekta ya umeme nchini, Dkt.
Kalemani
aliwashukuru wajumbe kutoka AfDB kwa kufadhili miradi miwili ya umeme ikiwa ni
pamoja na ule wa ‘Electricity 5’ uliowezesha kupeleka huduma ya umeme katika
vijiji vitano uliokamilika miaka miwili iliyopita.
Pia
aliishukuru AfDB kwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme
kutoka Iringa hadi Shinyanga yenye urefu wa Kilomita 670 uliokamilika mwezi
Desemba mwaka jana.
Akibainisha
miradi ya umeme inayosubiri ufadhili ili iweze kutekelezwa Dkt. Kalemani alisema
kuna
mradi wa Malagalasi unaohitaji kiasi cha Dola za Marekani 149 milioni
utakaozalisha megawati 44.8 za umeme utakaowawezesha wakazi wa Kigoma kupata umeme.
Dkt.
Kalemani alitaja mradi mwingine ni pamoja na wa Kakono unaotarajia kuzalisha
kiasi cha Megawati 87 za umeme ambao utaambatana na Mradi wa Ujenzi wa njia ya
kusafirisha umeme yenye urefu wa kilometa 88.8 kutoka Kakono hadi Kyaka kwa
gharama ya dolla za Marekani 387 milioni.
Akielezea
uwezo wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika kuzalisha na kusambaza
umeme,
Dkt. Kalemani alisema Serikali inalifanyia shirika hilo mabadiliko makubwa ili
liweze
kuendana
na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kufikisha huduma ya umeme kwa
wananchi na kuongeza kuwa ifikapo 2020 asilimia 75 ya watanzania watakuwa
wamefikiwa na huduma ya umeme.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB anayeiwakilisha Afrika Kusini, Mmakgoshi Lekhethe
alisema wamefika katika kikao hicho ili kuweza kujua mipango na
changamoto katika uendelezaji wa Sekta ya Nishati na kufahamu uwezo wa TANESCO
katika kusimamia
miradi
iliyoainishwa ili kufungua fursa za kiuchumi katika Kanda ya Magharibi.
Aidha,
Mmakgoshi alieleza kuwa AfDB inatambua umuhimu wa Nishati katika kukuza uchumi
wa nchi
na kuongeza kuwa kama wadau wapo tayari kuhakikisha Sekta ya Nishati inakuwa na
mchango
mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
0 comments:
Post a Comment