Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT),Gratian Mukoba amesema wamepata wito kutoka serikalini ukiwataka machi 16 mwaka huu kukutana Mkoani Dododoma .Wito huo umekuja siku chache baada ya walimu kuanza mgogoro na serikali ,wakishinikiza kulipwa madai yao yanayofikia takribani sh.800 Bilion.
Akizungumza Dar es salaam jana ,Rais wa chama hicho Gratian mukoba alisema kuwa licha ya wito huo wataendelea na mgogoro huo na Serikali hadi watakapolipwa madai yao.Alisema ’’ tunaweza kutangaza kufanya maandamano kuuelezea huma na ulimwengu kuhusu madai yetu au kukaa bila kufanya kazi ,,alisema Mukoba .
Mukoba alisema kuwa walimu wanadai zaidi ya sh.300 billion ambazo ni kwa ajili ya kuwalipa stahiki za walimu walio pandishwa madaraja na walimu 80,000 walipandishwa madaraja kati ya januari na april 2016 hawajalipwa mishahara yao .
Madai mengine ni sh 480 billion za walimu wastaafu 6,044 wanadai fedha tangu mwaka 2012 hawajalipwa.
Pia, kuna walimu 39 elfu walipaswa kupandishwa madaraja mwaka huu wa fedha kuanzia julai 2016 lakin hawajapandishwa hadi sasa .
Tayari naibu waziri wanchi ,ofisi ya Rais (TAMISEMI) , Suleiman jafo amenukuliwa akisema uhakiki wa deni sh million 10 umekamilika hvyo ataendelea na mchakato wa ulipaji .February 7 mwaka huu Chama cha walimu CWT kilitoa siku 21 kwa serikali kulipa madai ya walimu vinginevyo wangeanzisha mgogoro bila kutoa notisi nyingine .
0 comments:
Post a Comment