TUZO YA 'MO IBRAHIM'YAKOSA MSHINDI


Na Samwel Willy

Taasisi ya Kiafrika inayotoa tuzo za Utawala bora ya MO Ibrahim imetangaza kukosa mshindi kwa mwaka 2016, inayotoa kwa viongozi wa Afrika waliostaafu.

                   


Toka kuanzishwa kwake mwaka 2006, imepata washindi mara nne tu. Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo Salim Ahmed Salim amekirti kuwa vigezo vya tuzo hiyo ni vya juu, kuweka kumpata mshindi na kwa haki kabisa.

Tuzo hizo ziko wazi kwa kiongozi yeyote wa taifa aliyechaguliwa kidemokrasia, ambaye amestaafu ama kumaliza muhula wake madarakani na hupewa tuzo hiyo baada ya miaka mitatu toka kumaliza utawala wake.

Na mshindi akichaguliwa hupata kiasi cha dola milioni 5.
Nimezungumza na mchambuzi wa mambo Jenerali Ulimwengu, kutaka kujua kwa nini mara hii tena hakupatikana mshindi wa tuzo hiyo?
Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment