DOOH…! ALIYO YASEMA TIMBULO KUHUSU MAMA YAKE MZAZI NI NOUMAA…



Na.
 Melkiory Gowelle

Msanii nyota wa bongo fleva nchini, Ally Timbulo ‘Timbulo’  amefunguka mengi kuhusu ‘haso’ za maisha yake na kukiri kuwa daima hawezi kumsahau mama yake mzazi.

Akizungumza Jijini Dar es salaam mkali huyo wa ‘single’ ya nenda usisahau amesema kuwa kama isinge kuwa mama yake mzazi asinge tambulika katika ulimwengu wa muziki.

Ameeleza kuwa mzazi wake huyo ndiye anastahili kuwa malkia wa nguvu wa miaka yote kwake sababu ndiye mwanamke pekee ambaye upendo wake bado hajauona kwa mtu yeyote Yule.

“Ni kitu kikubwa zaidi, hakika kama isingekuwa mamangu ningesha feli muziki., kwanza hakupenda nifanye muziki, lakini kwa upendo wake aliniruhusu ns kunitia moyo katika hili kwa kuwa sikupenda kufanya kitu tofauti na muziki.” Alisema timbulo.

Timbulo amesema kuwa hatoweza kuusahau mwaka 2011 ambapo ulikuwa mwaka mgumu kwakwe mpaka ilimpelekea kukata tamaa juu ya muziki na kurudi kwao Mbeya lakini mama yake ndiye aliye mrudishs kwenye mstari.

“Mama alinisisitiza kuwa mtoto wa kiume huwa hashindwi maisha, unaanzaje kuacha kitu ulichopigania kwa muda mrefu? Mama aliniuliza na kutaka kulipa gharama za kurekodi ambapo hakuwa na kipato kikubwa” alisema Timbulo.

“lakini ilitokea bahati pale ambapo Suka alipo nipigia simu na kutaka tuonane ili tuachie nyimbo ya domo langu ambayo hakuisikiliza tangu nimpe ‘CD’ yake kwa muda wa miezi miwili nyuma, hivyo mamangu alinipa elfu 30 ya nauli na kuja kurecord wimbo ulio badilisha maisha yangu yote, hivyo anapotokea mwanamke kuniomba elfu 20, huwa naongeza 20 namrushia mamangu.

Share on Google Plus

About BASEMENT255

0 comments:

Post a Comment