NA TUZO
MAPUNDA
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amewaaswa wa wakazi wa Mkoa Lindi kufanya kazi kwa bidii ili
kujiletea maendeleo.
Maneno hayo yamesemwa leo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ilulu
mjini Lindi akiwa kwenye mwendelezo wa ziara yake katika mkoa huo.
Akizungumza na wakazi hao Magufuli aliwataka
wananchi kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa Mkoa huo unameneo mazuri yanayofaa kwa
kuzalisha mazao mbalimbali.
Alisema eneo la Mkoa wenu umebalikiwa kuwa na
utajiri mkubwa wa kulima mazao tofauti kama mpunga na kuwa chachu ya kukuza
uchumi wa familia zenu na kuacha tabia ya kusubiri msaada kutoka
serikalini.,,alisema Rais Magufuli.
Amewata wananchi hao kushirikiana kwa pamoja
na viongozi kutatua changamoto ili kuleta maendeleo ya kweli hususani katika
kuendeleza shughuli za kimaendeleo kwa kuwa maendeleo hayana chama.
Aidha amezungumzia suala la kutoa fedha milioni 50
,kwa kila kijiji na kuwataka kuunda vikundi vidogovidogo iliwapewe fedha hiyo
.
0 comments:
Post a Comment