KUNA
MENGI NYUMA YA MAREFA WETU JAMANI!!!!!
NA TAGATO JAMES TAGATO
Mwamuzi katika mchezo wa mpira wa miguu ananafasi kubwa, lakini pia ni
kiungo muhimu katika kuhakikisha anatafsiri
vizuri sheria 17 za mpira uwanjani.Mwamuzi huyu pia ni binadamu ndio manaa huwa
anakuwa na wasaidizi ili kuhakikisha anapunguza mapungufu yake pindi awapo
uwanjani.
Nchini kwetu Tanzania waamuzi wameonekana ni moja kati ya kikwazo sugu
kinacho kwamisha maendeleo ya soka letu,huku pia wakizibeba lawama nyingi sana
za mashabiki pamoja wa wadau wengi wa masuala ya mpira nchini.
Lakini kinacho nishangaza ni kwanamna gani tunawapa lawama watendaji wakati
hatujui ni mfumo upi unamfanya mwamuzi
kuwa na vigezo vya kuchezesgha ligi kuu?
Ngoja nkupe mfano wa soka la nchi ya Uingereza wao mpaka mwamuzi afikie
kuchezesha ligi kuu lazima apitie tena kwa performance ya hali ya juu kwenye
level zi sizo pungua kumi na moja tena kulinga na umri.
Lakini nchini kwetu ni rahisi
mno,yani kozi ya wiki mbili mazoezi kwa vitendo utachezesha daraja la tatu na
la nne, kisha unakwenda tena kozi una pandishwa hadi juu daraja la pili,la
kwanza na hatimaye ligi kuu.Sasa ukiutazama huu mfumo unaweza kuona ni namna
gani marefa wetu wanapitia njia raihisi kuchezesha michezo migumu.
Mbali
na mfumo lipo suala kubwa la maslahi,kiukweli hapa ndio soka letu limeoza
kabisaa.Kiukweli waamuzi hawa huishi katika mazingira magumu ya vishawishi vya
timu zetu ziinazo jiita kongwe.Hapa ndipo mwamuzi anapo jikuta anachukua jukumu
la kubeba lawama ilimradi maisha yake yasonge tu mana pesa wanayoipata haikidhi
mahitaji yao kiukweli.
Hapa
litakataliwa goli hapa utanyimwa penalty hapa utapewa umeme (yaani kadi nyekundu)
mala vile basi vulugu tupu lakini mwisho wa siku yeye anatoa maamuzi yake
kumbeba aliye weka mzigo mezani.
Lakini jingine na lenye mantiki kubwa ni ukweli utabakia pale pale kuwa
kama unajiendesha bila mtu wa kukuangalia nini na wapi unakosea, basi we utakuwa
wa kukosea kila siku mana unajua hakuna wa kukuliza.Lakini pale England wao
wana jopo la waamuzi na kimsingi hili hu shughurikia maswala mengi yanao wahusu
waamuzi lakini jopo hili huwa ndani ya FA
Kama unakumbuka sakata la mwamuzi Mike Dean kushushwa hadi ligi daraja
la kwanza badaa ya kuvurunda kweny michezo kama Liverpool alipiocheza na
Everton lakini pia akatoa kadi nyekundu isiyo halali kwa Soufiane Feghuli wa kati
Westham ilipo ikabili Manchester United.
Kwa wenzetu ni rahisi kutoa maamuzi haya baada ya
kupita mikanda ya mchezo husika lakini pia ripoti ya mwamuzi.Sasa huku kwetu
kwanza ripoti itafika sawa lakini je atawajibishwa?ngoja tusubiri ile ya juzi
si wote tuliiona lakini ile itapigwa chini kimya kimya mi yangu Macho tu.
0 comments:
Post a Comment