NA JOHN MARWA.
MSANII wa filamu nchini, Elizabeth Michael amekili kuwa
utangazaji ni moja ya kipaji chake, na yuko tayali kuingia kwenye tasnia ya
habari, ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu.
Lulu ni mmoja wa wasanii wakike wenye mafanikio katika
tasnia ya filamu hapa nchini, licha ya kuwa kwenye tasnia hiyo kwa muda murefu,
hivi karibuni tumemshudia akijihusisha nautangazaji, ushereheshaji wa matukio
mbalimali na baadhi ya makampuni ya mawasiliano hapa nchini.
“Ni kweli utangazaji ni moja ya kipaji changu lakini sio
kitu ambacho nimejikita sana kukifanya, ila ni kitu ambacho ni kipata kazi
ambayo ntaona itanifikisha sehumu fulani katika (carier) kimaslahi, na
kitaaluma nitafanya kwa sababu naweza na kipaji ninacho. Alisema Lulu.
Basement ikahitaji kujua mikakati ya kazi yake ya filamu mwaka 2017, alisema
hawezi kusema lolote ila atakuwa tayali kuzungumza baada ya miezi miwili ijayo
ila kwa sasa yuko chini na (management) yake na baada ya hapo ndo ataweka hadharani
mipango yake.
Akizungumzia sakata la madawa ya kulevya ambalo linaendelea
hapa nchini na ambalo limewahusisha baadhi ya wasnii, viongozi wa dini,
wafanyabiashara na wanasiasa, amesema hana chochote cha kuzungumza lakini
amewaasa Watanzania kuwa watulivu na kufuata sheria za nchi.
“Kuhusishwa ni tuhuma na ukihusishwa kuna taratibu ambazo
zinafuatwa ambazo zikisha fuatwa zitaonyesha kweli unahusika ama huhusiki, so
kwa yeyote ambaye anatuhiwa ni kumuomba Mungu tu na kusubili taratibu zifuatwe
lakini mwisho wa siku ukweli utajulikana kama mtu anahusika ama hahusiki”. Alisema
Lulu.
0 comments:
Post a Comment