Na. Melkiory Gowelle
Waziri wa
Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Mosses Nnauye amempongeza msanii
wa bongo fravour Ditto Lameck ‘Ditto’ kwa ubunifu wa mashairi makali ya wimbo
wa Moyo sukuma damu.
Akizungumza
Jijini Dar es salaam Nape amesema sio jambo rahisi katika muziki kufikiria kitu
tofauti na wengine na kutumia ubunifu wa kukiwasilisha katika jamii.
“Ni tatizo
lipo katika jamii, jambo lipo katika jamii, lakini namna unavyo liwasilisha
unatumia sanaa fulani, utaalam Fulani na ubunifu ambao unagusa akili za watu
mpaka wakakubali kuwa kazi ya moyo ni kusukuma damu, hivyo ukichanganya na
mambo mengine unasababisha matatizo.” Amesema Nape.
0 comments:
Post a Comment