Na Abdul Claus
MWANAMUZIKI wa miondoko ya Singeli hapa nchini Amani
Hamisi "Manfongo" amesema bado yupo imara katika kuendeleza Muziki
wake licha ya kuachana na Meneja wake G Maker.
Mwanamuziki huyo pia ameweka wazi kuwa lengo lake ni
kuhakikisha muziki wa Singeli unapasua anga mpaka kimataifa zaidi.
Akizungumza na Kituo kimoja Cha Runinga hapa nchini
Manfongo ameweka wazi kuwa Wala hajatetereka kwa lolote licha ya kuachana na
usimamizi wa G Maker kwani hata hapo awali Meneja Huyo alikuwa akitumia mapato
ya Maonyesho yake kumuendeleza kimuziki.
"Mimi mbona bado naendelea na harakati zangu za
kuuendeleza Muziki wa Singeli upige hatua labda kitu ulichokuwa hujui ni kwamba
G Maker alikuwa anatumia hela za maonyesho yangu kuniendeleza kimuziki
nimeangalia pia hilo nikaona naweza kujisimamia mwenyewe na mambo yakaenda
Vizuri tu"
Attachments area
0 comments:
Post a Comment