Na
Tuzo Mapunda
KATIBU mkuu wa timu ya Yanga Fc, Charles Bonifas Mkwasa
amekanusha taarifa zinazosema timu hiyo inaukata wa fedha.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya
taarifa kuzagaa kwenye vyombo vya habari zikisema timu hiyo imeshindwa kuwalipa
wachezaji wake mishahara yao.
AKizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo,
Mkwasa alisema timu hiyo haina ukata wa fedha na inaongoza kwa kulipa mshara
mzuri wachezaji wake ukilinganisha na klabu zingine hapa nchini.
"tuna uwezo wa kupeleka wachezaji kwenye hotel
yeyote hapa nchini na nje bila kujali gharama yeyote ukilinganisha na timu
zingine" Alisema mkwasa.Akasema kama kunamchezaji au mtu yeyote anaidai
timu hiyo basi atoe vielelezo vyake.
Hata hivyo amewaomba wapenzi na mashabiki wa timu ya
yanga kuiunga mkono timu yao kuelekea mechi za kimataifa na mashindano mengine
na kuachana na kusikiliza maneno yasiyokuwa ya msingi katika timu
yao.
0 comments:
Post a Comment