Na. Saphinia Suleimani
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO ) limetoa siku kumi na nne (14)
kwa wateja wake wote kuhakikisha wanalipa madeni yote wanayodaiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dakta.
Tito Mwinuka amesema kuwa shirika linawadai baadhi ya wateja
wake takribani shilingi billion 275, hivyo shirika linakusudia
kuendesha zoezi la ukusanyaji wa madeni ya bill za umeme
ambazo zimelimbikizwa na wateja mbali mbali nchi nzima.
Mwinuka
amesema kuwa madeni hayo yanajumuisha wateja wote wadogo,
Wizara, Mashirika ya umma, taasisi mbali mbali za serikali pamoja na
kampuni binafsi.
Hata hivyo amewataka wadaiwa wote
kulipa madeni yao ndani ya siku 14, huku akisisitiza huduma hiyo
itasitishwa endapo wateja watashindwa kulipa madeni yao.
0 comments:
Post a Comment