Na. Melkiory Gowelle
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekiri kuwa moja kati ya
changamoto kubwa ya kuwadhibiti maharamia wa kazi za wasanii nchini ni ukongwe
na ubovu wa sheria zilizopo.
Akizungumza
Jijini Dar es salaam Nape amesema kuwa sheria tulizo nazo ni za miaka ya sabini
ambayo haifanani na mazingira ya leo, hivyo anacho hangaikia hivi sasa ni
kutunga sera ya sanaa na sheria ambayo itasimamia vyema.
“Kwa mfano
hizi ‘operation’ ninazo zifanya mtaani, unamkuta mtu anakazi za bilioni mbili,
unampeleka mahakamani analipa faini laki mbili, unajiuliza kazi niliyo fanya ni
nini?, nimempeleka mahakamani, nimemkamata na kazi za wasanii za shilingi
bilioni tatu, juzi nimemkamata mtu ana billion 3 na zaidi.” alisema Nape na
kuongeza
“Kwa hiyo
huyu atatenga hiyo hela tuu ambayo mkienda mahakamani analipa, anarudi
anaendelea tena kwa hiyo sheria tuliyo nayo kwa kweli ni mbovu sana na ndiyo
inayo vunja moyo sana, lakini pamoja na ubovu wake ni lazima tusimamie,
tupunguze huu wizi wa kazi za sanaa zinazo endelea mtaani.” Alisema Nape
0 comments:
Post a Comment