Na. Melkiory Gowelle
Wekundu wa
Msimbazi ‘SIMBA’ wamepokea na kuukubari mwariko wa Chama Cha Mpira wa Miguu
mkoani Dodoma (DOREFA), hivyo weekend hii watakuwa huko kukipiga mechi ya
kirafiki dhidi ya miamba ya mkoa huo ‘Polisi Dodoma’.
Akizungumza
Jijini Dar es salaam Makamu wa klabu hiyo Geofrey Irick Nyange Kaburu ‘Perez’ amesema
kuwa mechi hiyo itakuwa mahususi kabisa kwaajili ya wapenzi wao wa Dodoma na
wageni wote waliokuwa wamehamia mkoani hapo.
“Tuna wapenzi wengi mkoani Dodoma kwa hiyo
itakuwa hasa ni kwaajili ya kuwapa furaha na vile vile kuiona timu yao,
ukizingatia kwamba wiki ijayo hatuna ratiba yeyote hivyo tutaitumia fursa hii
kuwa na wanachama wetu kule Dodoma” amesema Kaburu.
Aidha Kaburu
amesema watautumia mchezo huo kama moja ya maandalizi ya mechi ya robo fainali
ya Azam Sports Federation Cup ‘FA’ itakayo fanyika mwishoni mwa wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment