NA TUZO MAPUNDA.
Mabingwa wa tetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara Yanga Fc imelazimisha sare ya kutokufungana na Mtibwa sugar katika mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom .
Mchezo huo ulipigwa leo katika dimba la uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro ambapo Mtibwa sugar FC waliwakaribisha wanajangwani hao.
Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali uku kila timu ikitamani kufumania nyavu ya mwenzake dakika za mapema uku mashambulizi yakitokea kila upande .
Kufikia dakika ya dakika 37 mshambuliaji wa yanga Simoni Msuva alikosa mkwaju wa penati baada ya beki wa Mtibwa Aliy Lundenga kunawa mpira kwenye eneo la hatari. Hadi kipindi cha kwanza kinakamilika timu zilienda mapumuziko zikiwa azijafungana.Kipindi cha pili kilianza kwa washambuliaji wa mtibwa kulishambulia lango la Yanga Mara kwa mara lakini juhudi zao hazikuweza kuzaa matunda uku timu ya yanga wakishambulia kwa zamu hadi mchezo unakamilika milango ya timu zote mbili ilikuwa migumu.
Katika mchezo huo kila timu ilifanya mabadiliko lakini haya kuzaa matunda yeyote.Refa wa mchezo huo alikuwa Hamed kikumbo kutoka Dodoma
Kikosi cha yanga leo kiliundwa na Kocha George Lwandamina ,Hassan Kessi,Simon Msuva,Oscar Joshua,Kelvin Yondani,Degratias Munishi,Justin zulu,Emmanuel Maltrin,Harub Kanavaro,Malimi Bussungu,Jofrey mwashuya,Obrwe Shirwa,Hassani Hamis,Said Juma,
Kwa upande wa Mtibwa kikosi kiliongozwa na kocha Zuber katwila,Ally Lundenga,Shaban Nditi,Said mwamed,Hissa Rashid,Jaffari Salum,Stamili Mbonde ,Ally Makarani,Aruna Chanongo,Kelvin Fraiday
Kwa matokeo hayo Timu ya Simba bado wapo usukani mwa Ligi wakiwa na pointi 55 wa kifuatiwa na yanga wenye point 51.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment