Na. Melkiory Gowelle
Timu ya soka ya Chelsea imezidi kuongeza kasi katika mbio za
kuwania ubingwa wa ligi kuu nchini England ‘EPL’ msimu huu baada ya kuwachabanga
mahasimu wao wakubwa West Ham United mabao 2-1.
The blues ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao katika
mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Olympic stadium (uwanja wa nyumbani wa
West Ham) kupitia kwa winga wake matata Eden Hazard akiunganisha pasi safi
kutoka kwa Pedro katika dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, tayari
Chelsea walikuwa wako mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote
zikishambuliana kwa zamu, lakini Whest Ham walionyesha utulivu mkubwa katika
kumiliki mpira huku wakilifikia lango la Chelsea mara kwa mara, kabla ya Diego
Costa kuiandikia Chelsea bao la pili
katika dakika ya 50 akimalizia vyema kona iliyo chongwa na kiungo
mhispania Cecs Fabregas.
Bao pekee la West Ham
lilifungwa katika dakika ya 92 kupitia kwa winga wake wa kulia Lanzini
akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Andre Dede Ayew.
Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufikisha alama 66 katika
mechi 27 ilizo cheza na kushikilia nafasi ya kwanza, huku Totenham ikiwa nafasi
ya pili kwa alama 56 alama 10 nyuma ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment