Serikali imewataka
wazazi na walezi wa wanafunzi wanao hitimu kidato cha sita kuwa ruhusu watoto wao
kujiunga na jeshi la kujenga Taifa JKT.
Wito huo umetolewa
na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na ufundi stadi Profesa Joyce Ndalichako.
Akizungumza Jijini
Dar es salaam Ndalichako amesema, mafunzo ya miezi mitatu ya ukakamavu yanayo
jumuisha mambo mbalimbali kama vile mafunzo ya uzalishaji mali na kuisha pamoja
ni vitu vizuri vinavyo leta usawa na uzalendo.
“mipango ya
kwenda JKT bado inaendelea, nilipata bahati ya kukaribishwa kuwa mgeni rasmi
katika kambi ya Ruvu wakati hawa wa ‘Operation’ Magufuli wakiwa wanamaliza kile
nilicho kiona ni kitu kizuri sana na mimi ningetoa wito wa wazazi wawaache
watoto waende JKT.” Alisema Ndalichako.
0 comments:
Post a Comment