Na Tagato James Tagato
Mshambuliaji mwenye asili ya Ubeligiji na klabu ya
Chelsea fc Eden Hazard amemmwagia sifa mchezaji mwenzie N’golo Cante akimtaja
kama ni moja kati ya viungo bora.kauli hiyo ameitoa alipokuwaz akihojiwa baada
ya mchezo uliowakutanisha na Westham na ukamalizika kwa Chelsea kuibuka na
ushindi wa goli 2-1.
Hazard alisema “yeye(Cante)ni moja kati ya viungo bora na
wakati mwingine huwa najihisi nacheza na pacha wangu uwanjani nikiwa nae”
Sifa hizi zimekuja baada ya Cante kutoa mchango mkubwa
kwenye goli la kwanza lililofungwa na Eden Hazard katika dakika ya 25 ya mchezo
huku pia akiwa muhimili muhimu katika
safu ya ulinzi wa timu hiyo.
Alipo ulizwa kuhusiana na mchezo huo Hazard alisema “hakika
hatukucheza mchezo mzuri lakini tulijilinda vizuri na tulistahili ushindi”
Sasa Chelsea anakaa kileleni mwa msimamo wa EPL (English premier
league)kwa tofauti ya alama 10 huku ikiwa imesalia michezo 12 pekee ili ligi
hiyo ifikie tamati
0 comments:
Post a Comment